Al-Shabab "wagawa chakula Somalia"

Al-Shabab wagawa chakula Somalia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Al-Shabab wagawa chakula Somalia

Huku mashirika ya kutoa msaada yakiombia misaada wa dharura kwa waathiriwa wa ukame nchini Somalia, kundi la al-Shabab linasema kuwa limekuwa likigawa chakula kwa wale wanaohitaji.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa Somalia iko kwenye hatari ya kukumbwa na njaa, wakati watu milioni 6 ambao ni zaidi ya nusu ya watu nchini humo wakihitaji msaada.

Al-Shabab wamekuwa wlkipinga vikali kazi ya mashirika ya kutoa misaada nchini Somalia, hata ile ambayo inahusu ukame.

Kundi hilo linayalaumu mashirika hayo kwa kugawa chakula kilicho na kemikali ambazo husababisha magonjwa.

Kwenye taarifa zake kupitia mitandao na redio, kundi hilo sasa linasema kuwa wanamgambo wake wamekuwa wakigawa maji, unga wa ngano, mchele, sukari na mafuta ya kupikia kwa wale wanaokumbwa na ukame nchini Somalia.

Haijulikani ni wapi al-Shabab wanakitoa chakula hicho. Wanadai kuwa wananbunua chakula hicho kutoka kwa masoko lakini huwa wanafahamika kwa kuwotosa ushuru watu na kupora kutoka kwa wanavijiji ambapo watu wanawapinga.

Wakati wa njaa mwaka 2011 , wanamgambo hao walizuia usafirishaji wa misaada na kuwashambulia watoa misaada.