Marekani na Ujerumani kushirikiana kukuza uchumi wa dunia

Steven Mnuchin aliapishwa kuchukua nafasi hiyo mapema mwezi huu
Image caption Steven Mnuchin aliapishwa kuchukua nafasi hiyo mapema mwezi huu

Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin amesema atafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na waziri mwenzake wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble ili kuhakikisha kuwa uchumi wa dunia unakua kwa kasi sambamba na kuimaisha zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Berlin ikiwa ni ziara ya kwanza ya Mnuchin barani Ulaya tokea kuteuliwa kushika wadhifa huo akiwa pia anaenda kuhudhururia mkutano wa nchi 20 zinazoongoza kwa viwanda duniani utakaofanyika siku ya Ijumaa.

Image caption Wolfgang Schaeuble amekuwa waziri wa fedha Ujerumani tokea mwaka 2009

Ujerumani ni miongoni mwa nchi za Ulaya zinazofanya biashara kwa kiwango kikubwa na Marekani.

Steven Mnuchin was sworn in as Treasury Secretary earlier this month