Maseneta Marekani: Majengo ya Trump hayakupelelezwa na Obama

Moja ya majengo yanayomilikiwa na Rais Trump
Image caption Moja ya majengo yanayomilikiwa na Rais Trump

Viongozi wa kamati ya maseneta wa Republican na Democratic Richard Burr na Mark Warner wamesema hakuna dalili yoyote inayoonyesha kuwa majengo ya Trump yalikuwa yakifuatiliwa kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mwenyekiti wa tume ya uchunguzi amesema pia hakuamini madai hayo yaliyotolewa na Rais Trump dhidi ya mtangulizi wake Barack Obama.

Katibu wa Rais Trump Sean Spicer amesema uchunguzi haujafanyika vya kutosha juu ya suala hilo.

Image caption Awali Trump alimtuhumu Obama kuwa anamfanyia upelelezi

Hakuweka wazi kuwa ni taarifa za aina gani ambazo bado hazijawekwa wazi.