Syria:Watu 40 waliuawa katika shambulizi la msikiti

Mpaka sasa hakuna aliyetaja kufanya shambulizi hilo
Image caption Mpaka sasa hakuna aliyetaja kufanya shambulizi hilo

Wanaharakati wanasema kuwa takriban watu 40 waliuawa wakati msikiti mmoja Kaskazini Mgharibi mwa Syria ulipolipuliwa na ndege za kivita ambazo hazikufahamika.

Muangalizi mmoja wa haki za binaadam nchini Syria anayetokea nchini Uingereza amesema msikiti huo ulishambuliwa wakati watu wakiwa kwenye swala ya alasiri.

Kundi moja la wafuatiliaji wa mambo linasema msikiti huo ulikuwa katika eneo ambalo linashikiliwa na waasi.

Jeshi la Marekani linasema siku ya Ahamis liliwaua baadhi ya wapiganaji wa Al Qaeda kwa kutumia ndege za kivita wakati wakiwa kwenye kikao chao eneo moja liitwalo Idlib.

Taarifa hiyo haijataja kuwepo kwa vifo ama kujeruhiwa kwa wananchi wa kawaida.