Peru yatoa tahadhari kufuatia mvua kubwa

Mwanamke huyu alizamishwa na mafuriko ambayo bado yanaendelea
Image caption Mwanamke huyu alizamishwa na mafuriko ambayo bado yanaendelea

Mamlaka nchini Peru imetoa tahadhari kwa raia wa nchi hiyo kufuatia mvua kubwa iliyosababisha mmomonyoko wa ardhi huku mito miwili ikijaa kupitiliza na maji kuingia katika makazi ya watu katika mji mkuu wa Lima.

Shule na barabara nyingi zimefungwa.

Zaid ya watu 60 wamekufa kwa mafuriko nchini Peru tokea mwezi Desemba huku maelfu wakipoteza makazi yao.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kupata joto kwa bahari ya Pacific kupitiliza ni sababu moja wapo ya mvua hizo na kuongeza kuwa zitaendelea kwa majuma kadhaa.