Shirika la ujasusi Uingereza lakana kumdukua Trump

Mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza, G-C-H-Q, imetoa taarifa, kukanusha kuwa ilimdukua Bwana Trump wakati wa kampeini ya uchaguzi mkuu nchini Marekani.
Image caption Mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza, G-C-H-Q, imetoa taarifa, kukanusha kuwa ilimdukua Bwana Trump wakati wa kampeini ya uchaguzi mkuu nchini Marekani.

Mamlaka kuu ya mawasiliano ya kiintelijensia nchini Uingereza, G-C-H-Q, imetoa taarifa, kukanusha kuwa ilimdukua Bwana Trump wakati wa kampeini ya uchaguzi mkuu nchini Marekani.

Msemaji wa mamlaka hiyo anasema kuwa, madai yanayoashiria kuwa Uingereza ilitekeleza hatua hiyo , huku akinukuu tamko la msemaji wa Ikulu ya White House Bwana Sean Spicer, kama "matamshi ya kutamausha".

Madai hayo yaliyotolewa na mtangazaji mmoja wa Marekani, Andrew Napolitano, yalionekana hapo jana Alhamisi na msemaji wa Ikulu ya White House, Shon Spicer.

Rais Trump anadai kuwa mtangulizi wake Barrack Obama aliamuru kurekodiwa kwa mawasiliano ya simu zake zote.

Lakini viongozi wa vyama vya Republican na Democratic ndani ya kamati maalum ya ujasusi katika bunge la Seneti, wanasema hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa Trump Tower ililengwa na majasusi wa nchi hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii