Barcelona kuikabili Juventus, Real Madrid dhidi ya Bayern

Wachezaji wa leicester wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Sevilla. Timu hiyo inakutana na Atletico Madrid
Image caption Wachezaji wa leicester wakisherehekea ushindi wao dhidi ya Sevilla. Timu hiyo inakutana na Atletico Madrid

Leicester City itakutana na klabu ya Uhispania Atletico Madrid katika robo fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Mabingwa hao wa ligi ya Uingereza walisonga na kuingia katika robo fainali ya mchuano huo baada ya kuishangaza miamba wa Uhispania Sevilla 3-2 kwa jumla.

Leicester itacheza awamu ya kwanza ya mechi hizo nchini Uhispania mnamo tarehe 11 ama 12 ya Aprili huku mechi ya marudiano ikichezwa kati ya tarehe 18 na 19 ya Aprili.

Mabingwa watetezi Real Madrid watakutana na Bayern huku Barcelona wakimenyana na Juventus.

Borussia Dortmund kutoka Uingereza itacheza dhidi ya Monaco.

Atletico Madrid (Spain) v Leicester City (Eng)

Borussia Dortmund (Germany) v Monaco (France)

Bayern Munich (Germany) v Real Madrid (Spain)

Juventus (Italy) v Barcelona (Spain)