Wakazi Japan wajiandaa dhidi ya shambulio la Korea Kaskazini

Wakaazi wa Japan wajiandaa dhidi ya shambulio lolote la Korea kaskazini
Image caption Wakaazi wa Japan wajiandaa dhidi ya shambulio lolote la Korea kaskazini

Wakaazi wa mji mmoja ulioko kaskazini magharibi mwa pwani ya Japan, wameendesha zoezi la kukabliana na hali ya hatari na kujiandaa kwa shambulizi la aina yoyote, ikiwa Korea Kaskazini itaamua kuwashambulia kwa makombora.

Zaidi ya watu 100 walihusika katika zoezi hilo lililofanyikia maeneo ya Oga huko Akita, kwa kukimbilia hifadhi shuleni na katika vituo vya kuwahudumia jamii.

Walipokea tahadhari kupitia simu zao za mkononi.

Mapema mwezi huu, makombora matatu ya Korea Kaskazini yaliangushwa katika maeneo ya maji yaliyoko pwani ya Japan.

Mada zinazohusiana