IOM: Wakimbizi 30 kutoka Somalia wauawa

Miili ilisombwa na maji na kusafirishwa hadi ufukweni
Image caption Miili ilisombwa na maji na kusafirishwa hadi ufukweni

Shirika la kimataifa linaloshughulikia maswala ya uhamiaji IOM limethibitisha

Zaidi ya wakimbizi 30 kutoka Somalia walioko Yemen wameuawa katika shambulio lililolenga boti waliokuwa wakisafiria wakiwa kwenye bahari ya Shamu.

Vikosi vinavyoshughulikia doria za baharini katika bandari ya Hodeidah inayodhibitiwa na waasi Wa-houthi vinasema boti hilo lilikuwa linatoka Yemen kuelekea Sudan wakati liliposhambuliwa kwa kombora.

Kituo cha habari kinachomilikiwa na waasi hao kimedai shambulio hilo limefanywa na ndege ya hlikopta aina ya Apache .

Zaidi ya majeruhi 80 wa mkasa huo wamekimbizwa hosptialini.

Eneo la Hodeidah ni mojawapo linalokumbwa na mashambulio ya mara kwa mara kutokana na mzozo wa kivita unaoendelea baina ya jeshi la Yemen linaloungwa mkono na lile la Saudia, dhidi ya waasi hao wa Houthi wanaopinga serikali ya Yemen.