Ikupa Mwambenja:Nitasaidia tasnia ya muziki wa Injili

Image caption Ikupa Mwambenja

Ikupa Mwambenja mwimbaji Chipukizi wa Muziki wa Injili kutoka mkoa wa Mbeya-Kusini Magharibi mwa Tanzania.

Vikwazo kadhaa alivyovipitia akijaribu kung'ara ndivyo vinavyomsukuma kutaka kuwasaidia wengine atakapokifikia kilele cha mafanikio.

"Kuna wakati nilikuwa nalazimika kutembea kwa umbali mrefu kwenda kutafuta sehemu ya kurekodi, ninafahamu kuwa hata wasanii wengine chipukizi wanaipitia hali hii. Ni ngumu Zaidi kwa watoto wa kike"Anasema Ikupa.

Hivi ndivyo Ikupa Mwambenja alivyomweleza mwandishi wetu Arnold Kayanda.