Ndege zagongana nchini Canada

Ndege zagongana nchini Canada
Image caption Ndege zagongana nchini Canada

Ndege mbili zimegongana zilipokuwa katika anga ya eneo moja la shughuli nyingi za kibiashara huko nchini Canada.

Rubani mmoja amefariki na mwengine kureruhiwa vibaya sana.

Police wanasema hata ni miujiza kwamba hamna mtu mengine yeyote aliyejurihiwa licha ya ndege moja ya hizo kuanguka juu ya paa la mojawapo ya maduka makubwa la eneo hilo nje kidogo mwa mji wa Montreal.

Ndege nyengine ilianguka eneo la kuogesha magari.

Ndege zote ni za aina ya Cessnas kutoka shule moja ya ufunzi wa urubani - Hali hmbaya ya hewa ndio unadhaniwa kusababisha ajali hiyo.