G20: Marekani na China kuongoza mjadala wa biashara huru

Mkutano wa G20 Ujerumani: Marekani na China kutofautiana kuhusu sera huru ya biashara
Image caption Mkutano wa G20 Ujerumani: Marekani na China kutofautiana kuhusu sera huru ya biashara

Mkutano wa mataifa taifa 20 tajiri zaidi dunani Uitwao G20 unafanyika huko Ujerumani , ukiwahusisha mawaziri wa fedha na wasimamizi wa mabenki kuu ya nchi hizo.

Taarifa yao inasubiriwa kwa hamu kuona iwapo watakuwa wameunga mkono sera za biashara huru au la.

Katika kikao kama hicho hapo miezi minane iliyopita Uchina iliunga mkono kwa dhati sera hiyo ya biashara huru ambayo imeifaidi pakubwa kwa kuweza kuuza bidhaa zake kwa wingi kote duniani.

Hata hivyo utawala wa sasa wa Marekani chini ya rais Trump umesema utaweka vizingiti vikali vya ushuru kulinda zaidi biashara za Marekani .

Pia amesema ataibatilisha mikataba ambayo anasema haijaifaidi Marekani.