Manchester United yawatandika Middlesbrough 3-1

Manchester United yawatandika Middlesbrough 3-1 Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Manchester United yawatandika Middlesbrough 3-1

Manchester United walipiga hatua mbele hadi nafasi ya tano katika jedwali kwenye Premier League walipoilima Middlesbrough mabao 3-1.

Pasi safi ya Ashely Young ilipokelewa na Marouane Fellaini, ambaye alitumbukiza mpira wavuni baada ya Jesse Lingard kutikiza wavu katika kipindi cha pili.

Hata hivyo Middlesbrough waliwavamia Man U baada ya Chris Smalling kufanya kosa ambapo alimpa Rudy Gestede nafasi wazi ya kufunga.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho sasa kimewapiku Arsenal and Everton hadi nafasi ya tano huku Middlesbrohg wakibaki katika nasafi ya 19.