Wenger kutangaza hatma yake hivi karibuni

Arsene Wenger Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsene Wenger

Hivi karibuni Meneja wa Arsenal Arsene Wenger atatangaza ikiwa atasalia Arsenal baada ya kufanya uamuzi wa hatma yake.

Wenger alikuwa akizungumza baada ya Arsenal kushindwa kwa mabao 3-1 na West Broms ambacho ni kipigo cha nnne kwa miaka mitano.

Kushindwa huku kulimuongezea shinikizo Wenger na kuiacha Arsenal katika hatari ya kushindwa kumaliza katika nafasi ya timu nne za kwanza kwa mara ya kwanaa kabisa tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 1996.

"Ninajua kile nitakifanya, hivi karibuni mtajua." alisema Wenger.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mashabiki wamekuwa wakibeba mabango ya kumtaka Wenger kuondoka

Mkataba wa Wenger unakamilika mwishoni mwa msimu lakini tayari ashaongezewa mkataba mpya wa miaka miwili.

Amekabiliwa na shinikizo siku za hivi karibuni huku mashabikia wakilalamikia kushindwa kwa Arsenal kwenye Premier League, na kushindwa na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 10-2 katika Champions League na kumtaka aondoke.

"Nafikiri tuna kazi kubwa lakini tunahitaji kuungana na kuangazia mechi zinazokuja, kwa sababu tuna mechi kubwa," Wenger alikiambia kituo cha Sky Sports.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Arsenal walishindwa kwenye Premier League, na pia kushindwa na Bayern Munich kwa jumla ya mabao 10-2 katika Champions League