Vikosi vya Syria vyapambana na waasi mjini Damascus

Kumekuwa na mapambano makali nchini Syria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kumekuwa na mapambano makali nchini Syria

Kumekuwa na mapambano makali kati ya vikosi vya serikali ya Syria na waasi mashariki mwa mji wa Damascus.

Mapambano hayo ya yalifanyika baada ya shambulizi la kushtukiza karibu na katikati ya mji lililotekelezwa na waasi kutoka kundi linalohusishwa na wanamgambo wa al-Qaeda.

Vyombo vya habari vya serikali vimesema mahandaki yalitumika kufanya shambulizi hilo.

Shirika la kutetea haki za binaadam lenye makazi yake nchini Uingereza limesema wanamgambo walilipua mabomu yaliyokuwa yametegwa kwenye gari kabla ya kushambulia vizuizi vya kujihami .

Jeshi la Syria lilirudisha mashambulizi kwa njia ya anga.

Wakazi waliaswa kubaki ndani, huku shule zikitarajiwa kuendelea kufungwa