Waliopanga mauaji dhidi ya Rais wa Honduras kuhukumiwa

Rais Hernandez amekuwa akipambana na makundi ya uhalifu na biashara ya Dawa za kulevya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Hernandez amekuwa akipambana na makundi ya uhalifu na biashara ya Dawa za kulevya

Mahakama nchini Honduras imewakuta na hatia watu watatu wanaojishughulisha na magenge ya biashara ya dawa za kulevya kwa kosa la kupanga mipango ya kumuua Rais wa nchi hiyo, Juan Orlando Hernandez baada ya uchaguzi mwaka 2014.

Waendesha mashtaka wamesema amri ya kumuua rais ilitoka kwenye genge liitwalo de los Valle, nchini Honduras na kundi jingine kutoka Mexico la Sinaloa, linaloongozwa na Joachim maarufu 'El Chapo' Guzman.

Bwana Hernandez aliongoza kwa miaka kadhaa Kampeni dhidi ya makundi ya uhalifu yanayofanya biashara ya dawa za kulevya.

Watu hao watatu, wawili raia wa Mexico, mmoja wa Honduras watahukumiwa mwezi ujao.