Man City , Liverpool hakuna mbabe

Sergio Aguero amefunga goli moja katika kila mechi dhidi ya Liverpool uwanja wa Etihad, na kufikisha magoli matano Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sergio Aguero amefunga goli moja katika kila mechi dhidi ya Liverpool uwanja wa Etihad, na kufikisha magoli matano

Manchester City imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa Etihad baada ya kukubali sare ya bao 1-1 na Liverpool.

Beki wa kushoto wa Liverpool James Milner ndiye aliyeanza kuiandikia timu yake bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 51 ya mchezo.

Katika dakika ya 69 mshambuliaji wa Man City Sergio Aguero akaisawazishia timu yake baada ya kupokea krosi nzuri toka kwa kiungo Kevin de Bruyne's.

Baada ya matokeo ya mchezo huo City inasalia katika nafasi ya tatu kwa alama 57 wakiwa wamecheza michezo 28, huku Liverpool wakiwa katika nafasi ya nne kwa alama 56 na michezo 29.