Azam Fc nje kombe la shirikisho

Kikosi cha Azam Fc Haki miliki ya picha Google
Image caption Kikosi cha Azam Fc

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la wawakilishi klabu ya Azam Fc imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa kwa mabao 3-0 na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Mchezo huu ulikua ni wa pili wa raundi ya mtoano wa michuano ya kombe la shirikisho katika mchezo wa kwanza Azam walishinda kwa bao 1-0 wanaondolewa kwa jumla ya mabao 3-1.

Mbabane Swallows sasa wametinga raundi ya mchujo ya mashindano hayo shirikisho barani Africa.