Mhandisi aliyepewa jina Saddam Hussain akosa kazi

Saddam Hussein Baghdad, 18 October 1995 Haki miliki ya picha AP

Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Iraq Saddam Hussein ambaye ingawa alipingwa sana na baadhi ya watu, alipendwa sana na wengine.

Saddam ameendelea kuathiri maisha ya watu, hasa waliopewa jina lake.

Mmoja aliyeathirika ni mhandisi wa masuala ya baharini Saddam Hussain ambaye alipewa jina hilo na babu yake miaka 25 iliyopita Saddam Hussein alipokuwa bado ni maarufu.

Lakini Hussain ametatizika sana kutafuta kazi, jambo ambalo anaamini linatokana na jina lake, ingawa kuna tofauti kidogo kwamba anaitwa Hussain badala ya Hussein.

Anasema ametafuta kazi mara 40 bila mafanikio.

Kwa sasa, amewasilisha kesi mahakamani kujaribu kubadili jina lake awe akiitwa sasa Sajid.

Shughuli hiyo hata hivyo ilichukua muda mrefu.

Saddam Hussain alifuzu kutoka chuo kikuu cha Noorul Islam, Tamil Nadu miaka miwili iliyopita.

Yeye ni mzaliwa wa Jamshedpur katika jimbo la Jharkhand, mashariki mwa India.

Alifanya vyema chuoni lakini anasema wenzake chuoni wamepata kazi lakini yee hajabahatika.

"Watu huogopa kunipa kazi," anasema Saddam, na kuongeza kwamba huenda kampuni zinaogopa kwamba atatatizika kusafiri nje ya nchi hiyo.

Alifikiria huenda angetatua tatizo hilo kwa kupata pasipoti mpya, leseni ya udereva na nyaraka nyingine akitumia jina lake mpya la Sajid.

Lakini sasa vyeti vyake havilingani majina.

Ana kikao na mahakama 5 Mei kutaka kuwashurutisha maafisa wa elimu kubadilisha jila la vyeti vyake vya shule.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii