Rais wa Uber Jeff Jones ajiuzulu

Kuondoka kwa rais kumewashangaza maafisa wakuu wa Uber Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kuondoka kwa rais kumewashangaza maafisa wakuu wa Uber

Rais wa kampuni ya Uber Jeff Jones, amejiuzulu kutoka kwa kampuni hiyo chini ya miezi sita tangu achukue wadhifa huo.

Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo ya Texi ziliiambia Bbc kuwa, hatua hiyo ya kujiuzulu haikutarajiwa kabisa.

Iliripotiwa kuwa Jones alighadhabishwa kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikimuajiri afisa mkuu msimamishi wa huduma, na kuwa hakuwa miongoni mwa watahiniwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkurugenzi mkuu wa Uber Travis Kalanick naye huenda akang'atuka

Lakini kwa mujibu wa mtandao wa teknolojia, Recode, bwana Jones aliondoka kwa sababu ya masuala yanayoikumba Uber kwa misingi ya ubaguzi wa kijinsia na dhuluma za kimapenzi.

Kwenye taarifa yake siku ya Jumapili Uber ilisema, "Tungependa kumshukuru Jeff kwa kipindi cha miezi sita amekuwa na kampuni na tunamtakia mazuri."

Hata hivyo kampuni hiyo imeshangazwa na kuondoka kwake kwa ghafla , huku maafisa wengine wakiachwa na butwaa wa kutojulishwa kuhusu mipango yake.

Mada zinazohusiana