Mitambo ya kutambua watu inayotoa karatasi yawekwa kwenye vyoo China

Mitambo ya kutambua watu inayotoa karatasi yawekwa kwenye vyoo China
Image caption Mitambo ya kutambua watu inayotoa karatasi yawekwa kwenye vyoo China

Bustani moja nchini China imeweka mitambo ya kuwekwa karatasi za kutumika chooni, yenye uwezo wa kutambua uso wa mtu ili kuwazua wageni kutoa kiwango kikuwa cha karatasi za kutumika chooni.

Mashine hizo katika bustani ya Temple of Heaven hukagua uso wa wageni kabla ya kuachilia karatasi kwa kiwango kilichowekwa.

Bustani hiyo inayowavutia watalii inaripotiwa kutembelewa na watalii ambao hupeleka nyumbani kiwango kikubwa cha makaratasi ya kutumia chooni.

Image caption Mitambo ya kutambua watu inayotoa karatasi yawekwa kwenye vyoo China

Maafisa wa bustani sasa wameweka mashine sita kwenye choo za umma kwa majaribio ya nusu mwezi, huku wafanyakazi wakiwa karibu kuwalezea wageni kuhusu teknolojia hiyo.

Mashine hizo mpya hutumia vipande vya karatasi vyenye urefu wa kati ya sentimita 60 na 70 kwa kila mtu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wageni kwenye choo za bustani hiyo, walionekana wakichukua karatasi nyingi

Mashine hizo pia haziwezi kuachia karatasi kwa mtu mmoja hadi baada ya dakika tisa kuisha

"Ikiwa tutakabiliwa na wageni wanaoendesha au walio katika hali fulania wanaohitaji karatasi zaidi na chooni, wafanyakazi wetu watalishughulikia hilo moja kwa moja," msemaji wa bustani hiyo alisema.

Wakati BBC ilizuru bustani hiyo siku ya Jumatatu, mashine hizo zilikuwa zimezimwa. Mfanyakazi mmoja alisema kuwa hazikuwa zikitumika kwa sababu hakukuwa na wageni wengi bustani.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Mitambo ya kutambua watu inayotoa karatasi yawekwa kwenye vyoo China

Mapema mwezi huu vyombo vya habari nchini China, viliripoti kuwa wageni kwenye choo za bustani hiyo, walionekana wakichukua karatasi nyingi, ambapo hata wengine walionekana wakiziweka kwenye mikoba yao.

Usimamizi wa bustani hiyo sasa anasema kwa mfumo huo unaonekana kufanikiwa kwa sababu kiwango cha karatasi kinachotumiwa kimeshuka kwa asilimia 20.