FBI imethibitsha kuwa inachunguza madai kuwa Urusi iliingilia uchaguzi Marekani

Bwana James Comey (kushoto) na Mike Rogers mbele ya kamati ya bunge Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Bwana James Comey (kushoto) na Mike Rogers mbele ya kamati ya bunge

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani FBI James Comey, amethibitisha kwa mara ya kwanza kabisa kuwa FBI inaendesha uchunguzi wa madai kuwa Urusi iliingilia kati uchaguzi wa mwaka 2016.

Hii inahusu uchunguzi wa kuwepo uwezekano wa uhusiano kati ya watu kwenye kampeni ya Trump na serikali ya Urusi, na ikiwa kulikuwa ushirkiano kati ya kampeni ya Trump na Urusi.

FBI pia itachunguza ikiwa uhalifu ulifanyika. Trump hata hivyo amekana kuhusika kwa njia yoyote.

Urusi mara nyingi imekana majaribio ya kushawishi uchaguzi wa Marekani.

Mkurugenzi huyo wa FBI alikuwa akizungumza katika kikao kisicho cha kawaida cha kamati ya bunge la Congress, ambayo pia inachunguza uwezekano wa kuwepo ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.

Bwana Comey alisema kuwa uchunguzi huo ni mgumu na kuongeza kuwa hawezi kuipa kamati hiyo taarifa za kina ambazo bado hazijatolewa kwa umma.

Pia alisema kuwa hawezi kutoa tarehe ya kukamilika kwa uchunguzi huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Davin Nunes(kulia) mwenyekiti wa kamati ya ujususi pamoja na afisa wa Democrat Adam Schiff

Pia aliyefika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa sharika la kitaifa linalohusika na ulinzi NSA Mike Rogers.

Alisema kuwa NSA inaunga mkono ripoti iliyochapisjwa mwezi Januari, ambayo ilisema kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin, alikuwa ameamrisha harakati za kuvuruga kampeni za mshindani wa Trump, Hillary Clinton.

Maafisa wote hao pia walikana madai yaliyoandikwa kwenye mtandoa wa Twitter mapema mwezi huu na bwana Terump, kuwa rais wa zamani Barack Obama aliamrisha kufuatiliwa kwa mawasiliano kwenye jumba la Trump Tower.

Mwezi Januari mashirika ya ujasusi nchini Marekani yalisema kuwa Urusi iliwasaidia wadukuzi wa mitandao kudukua akaunti za barua pepe za maafisa wa juu wa Democrat ambao walifichua taarifa za aibu kumsaidia Trump kumshinda Hillary Clinton.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Trump amedai kuwa mawasiliano yake na ya chansela Angela Merkel yalifuatiliwa na Obama