Ndege ya abiria yaanguka Sudan Kusini

Ndege ya abiria yaanguka Sudan Kusini
Image caption Ndege ya abiria yaanguka Sudan Kusini

Kuna ripoti za kutatanisha kuhusu kilichosababisha kuanguka kwa ndege, kwenye uwanja wa ndege wa Wau kaskazini mwa Sudan Kusini

Ndege hiyo ya shirika la South Supreme Airlines, ilikuwa ikitua ikitokea mjini Juba.

Gavana wa jimbo wa eneo hilo Andrea Mayar Achor, aliiambia BBC kuwa kulikuwa na matatizo ya hali ya hewa.

Lakini mwandishi wa habari wa redio moja alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitoa moshi kutoka kwa mkia wake kabla ya kuanguka.

Idadi ya watu waliofariki au waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo nayo haijulikani.

Kulikuwa na takriban watu 40 ndani ya ndege hiyo lakini baadhi yao wanaripotiwa kunusurika.