Kvitova hajui lini atarejea uwanjani

Kvitova
Image caption Mcheza tenesi Petra Kvitova

Mcheza tenesi Petra Kvitova ambae alivamiwa mwezi Desemba mwaka jana na kukatwa na kisu mkononi ameweza kuanza kushika raketi ya kuchezea tenesi .

Lakini hata hivyo Kvitova hajui ni lini atarejea tena uwanja kuweza kucheza mchezo huo , tangu awali madaktari walisema itamchukua miezi sita kwa nyota huyo kuweza kurejea tena uwanjani.

Msemaji wa mchezaji huyo Karel Tejkal, amesema"Preta anaendelea vizuri na mkono wake unapona kama ilivyotarajiwa,"

Kwa sasa mchezaji huyo anaweza kuutumia mkono wake kama kawaida katika shughuli zake za kila siku na amekua akifanya mazoezi katika visiwa vya Canary