Man City kuadhibiwa na FA

Man City Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa Man City wakimzonga mwamuzi Michael Oliver

Klabu ya Manchester City, imeshitakiwa na chama cha soka cha nchini England FA, kwa kushindwa kuwathibiti wachezaji wake waliomzonga mwamuzi Michael Oliver, katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Hivyo Man city, wanaweza pigwa faini kwa kosa la hilo la wachezaji wake tukio hilo lilitokea baada ya mwamuzi kuipa Liverpoool, penati.

Oliver alitoa adhabu ya penati baada ya kuona Gary Clichy, amemfanyia madhambi Roberto Frimino, katika eneo la hatari, na mkwaju huo wa penati ukapigwa na James Milner aliyeukwamisha wavuni.

City wanatakiwa mpaka siku ya Alhamis kuwa wamepeleka utetezi wao kwa chama hicho cha soka cha England.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Man City

Oliver alikupatwa na kadhia ya kuzongwa na wachezaji wa Manchester united wiki iliyopita baada ya kumtoa nje kwa kadi nyekundu kiungo Ander Herrera katika mchezo wa kombe la FA kati ya Man United na Chelsea.