ulaya na China zasitisha uagizaji nyama toka Brazil

Brazil Haki miliki ya picha AP
Image caption Wabrazili wamekua na wasiwasi kuhusu ubora wa nyama wanazokula na kusambaza katika soko la dunia

China na Umoja wa ulaya ambao ni wateja wakubwa wa nyama toka Brazil,wamesimamisha uagizaji wa nyama kwa tuhuma kwamba makampuni yamekuwa yakiwauzia nyama ambazo sio salama kwa miaka mingi.

Nchi ya China imepiga marufuku kabisa uingizaji wa nyama nyekundu kutoka Brazil, wakati Umoja wa Ulaya ikitangaza kuacha kununua nyama, kuku na bidhaa nyingine kutoka makampuni yaliyohusika na kashfa.

Siku ya Ijumaa, polisi wa nchini Brazil walivamia ofisi kubwa za makampuni yanayozalishwa nyama na nchi humo

Makampuni hayo yametuhumiwa kuuza nyama iliyooza na kuwahonga waandamizi viongozi wa serikali.