FBI imethibitisha kuichunguza Urusi

FBI Haki miliki ya picha Google
Image caption Mkurugenzi wa FBI James Comey

Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani FBI James Comey, amethibitisha kwa mara ya kwanza kabisa kuwa FBI, inaendesha uchunguzi wa madai kuwa Urusi iliingilia kati uchaguzi wa rais.

Hii inahusu uchunguzi wa kuwepo uwezekano wa uhusiano kati ya watu kwenye kampeni ya Trump na serikali ya Urusi, na ikiwa kulikuwa ushirkiano kati ya kampeni ya Trump, na Urusi.

Mkurugenzi huyo wa FBI, alikuwa akizungumza katika kikao kisicho cha kawaida cha kamati ya mkutano wa bunge.

Ambacho pia inachunguza uwezekano wa kuwepo ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.FBI pia itachunguza ikiwa uhalifu ulifanyika. Trump hata hivyo amekana kuhusika kwa njia yoyote