Wenger ni mbinafsi amsema Sutton

Wenger Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Kocha wa Arsenal Arsene Wenger

Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Chelsea ya England, Chris Sutton, amesema kocha wa Arsenal Arsene Wenger ni mbinafsi kwa kuwa anaendelea kuwa kimya juu mustakabali wake wa kuendelea kuinoa Arsenal

Akizungumza na BBC Radio5 Sutton amesema Wenger ni kama Mjomba anayengangania kutokutoka katika tafrija. Na amekua akiirudisha timu nyuma siku zinavyozidi kwenda.

"Amekua akifeli katika nyakati za soko la usajili, fanya jambo sahihi kama huwezi tuambie huwezi ." ameeleza mchezaji huyo.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Chris Sutton

Wenger alianza kunioa klabu ya Arsenal toka 1996, na mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa ligi kuu ilikua ni mwaka 2004 na sasa timu inashika nafasi ya sita katika msimamo ligi.