Waziri 'ajishitaki' kwa Twitter kwa kutumia simu akiendesha gari

Waziri wa Australia aliyetumia simu akiendesha gari Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Waziri wa Australia aliyetumia simu akiendesha gari

Waziri wa polisi nchini Australia anasema kuwa hakujua kwamba alikuwa akivunja sheria wakati alipochukua simu yake akiwa anaendesha gari lake.

Troy Grant, mbunge mpya wa South Wales alichukua picha na kuichapisha katika ujumbe wa Twitter alipokuwa nyumbani.

Baada ya kuambiwa makosa yake ,bwana Grant alijiwasilisha katika kituo cha polisi ambapo alipigwa faini ya dola 250.

''Hii inawakumbusha watu kwamba hakuna mtu aliyejuu ya sheria ,alisema Grant''.

Waziri huyo alisimamishwa barabarani wakati alipopiga picha gari moja lililokuwa likibeba kondoo mbele yake.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Chapisho la Twitter lililowekwa na waziri huyo baada ya kuona kondo huyo

''Sikujua kwamba kile nilichokuwa nikifanya kilikuwa kinyume cha sheria, bwana Grant alisema siku ya Jumanne''.

''Hili ni funzo kwangu, na natumai ni swala ambalo jamii inachukua funzo''.

Chini ya sheria hiyo ,madereva wanaweza kutumia simu bila kuishika.

Mada zinazohusiana