Kundi la Hezbollah ladaiwa kumuua kamanda wake

Bedraddine anadaiwa kuuawa na jenerali mmoja wapiganaji waa kundi la Hezbollah Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bedraddine anadaiwa kuuawa na jenerali mmoja wapiganaji waa kundi la Hezbollah

Afisa mkuu wa jeshi la Israel ameongeza uzito katika vyombo vya habari vya Kiarabu kwamba kundi la wapiganaji wa Hezbollah lilihusika katika mauaji ya kamanda wake nchini Syria 2016.

Luteni jenerali Gadi Eisenkot alisema kuwa idara ya ujasusi ya Israel pia ilibaini kwamba Mustafa Amine Badreddine aliuliwa na wapiganaji wake.

Aliuawa katika mlipuko karibu na Damscus ambapo kundi la wapiganaji la madhehebu ya kishia lililaumu wapiganaji wenye itikadi kali wa Sunni.

Badreddine aliaminika kuendesha operesheni zake nchini Syria tangu 2011.

Hezbollah linahusishwa pakubwa katika vita vya wenye kwa wenyewe nchini humo, likiwa limesambaza maelfu ya wapiganaji ili kumuunga mkono rais Bashar al-Asaad.

Mapema mwezi huu, kituo cha habari cha al-Arabia kilisema kuwa uchunguzi wake mwezi huu kuhusu mauji ya Bedraddine ulibaini kwamba kamanda huyo aliuawa kutokana na agizo la Hassan Nasrallah.

Ripoti hiyo inasema kuwa Hassan Nasrallah alishinikizwa kumuua Bedraddine na meja jenerali Qasema Soleiman,kiongozi wa walinzi wa jeshi la Iran.

Mada zinazohusiana