Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani afika mbele ya wakuu wa mashtaka

Wafuasi wa Bi Park walikusanyika nje ya nyumba yake Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafuasi wa Bi Park walikusanyika nje ya nyumba yake

Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye anahojiwa na wakuu wa mashtaka, kufuatia sakata ya ufisadi ambayo ilisababisa atimuliwa madarakani.

Bi Park alipinga jitihada za kumhoji akiwa rais, lakini akapoteza kinga yake wakati majaji walipounga mkono uamuzi wa bunge kumuondoa madarakni.

Anashtakiwa kwa madai kuwa alimruhusu rafiki wake wa karibu Choi Sonn-sil kupata pesa kutoka kwa makampuni makubwa.

Bi Choi ameshtakiwa kwa makosa ya ulaji rushwa.

Wakuu wa mashtaka wanajaribu kumhoji Bi Park katika shughuli ambayo itaendelea hadi usiku.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bi Park ndiye rais wa kwanza wa Korea Kusini aliyechaguliwa kidemokrasia kulazimishwa kuondoka ofisini

Mmoja wa mawakili wake anasema kuwa madaktari wanamfayia uchunguzi wakati wa mapumziko kwa kuwa afya yake inaonekana kuwa isiyo nzuri.

Leo Jumanne wafuasi wa Bi Park walikusanyika nje ya nyumba yake katika mtaa wa kifahari wa mji wa Seol wakati alipokuwa akisindikizwa na polisi kuenda kwa ofisi za wakuu wa mashtaka kwenye safari fupi iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga.

Watu walipepusha bendera za Korea Kusini ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono.

"Ninaomba watu msamaha, nitatoa ushirikiano kwa mahojiano," Bi Park aliviambia vyombo vya habari alipowasili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Choi (katikati) analaumiwa kwa ulaji rushwa