Namibia kutwaa ardhi ya wazungu

Rais wa Namibia Hage Geingob Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Namibia Hage Geingob

Rais wa Namibia Hage Geingob, amelalamikia mwendo wa kinyonga wa mabadiliko katika sheria za umiliki wa ardhi, akisema kuwa serikali itashughulikia tatizo hilo kwa kutwaa ardhi na kuwalipa wamiliki wa kizungu fidia inayostahili.

Wakati wa hotuba ya kuadhimisha miaka 27 ya uhuru, bwana Geingob alisema kuwa serikali imetumia kila mbinu iliyo nayo kuwapa ardhi watu weusi kwa kutoa fursa kwa wale wanaouza na kununua kwa hiari.

Amesema kuwa serikali sasa itaitumia katiba ambayo inaruhusu kutwaliwa kwa ardhi kwa kulipa fidia inayoistahili na pia kwa kushughulikia ardhi inayomilikiwa na raia wa kigeni hasa wale hawapo.

Umiliki wa rdhi ni suala lenye utata kanda hiyo. Serikali ya Zimbabwe imekosolewa vikali na upanzani na mataifa ya kigeni kwa kutwaa ardhi iliyomiliwa na wazungu.

Nchini Afrika Kusini Rais Jacob Zuma, ametoa wito kutwaliwa kwa ardhi bila ya kulipa fidia lalini chama kinachoongoza kimependekeza ulipaji fidia ulio wa haki.