Marekani yazuia abiria kubeba vifaa vya eletroniki kutoka Misri na Morocco

Marekani yazuia abiria kubeba vifaa vya eletroniki kutoka Misri na Morocco Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani yazuia abiria kubeba vifaa vya eletroniki kutoka Misri na Morocco

Marekani imetangaza marufuku kwa vifaa vingi vya eletroniki kwa abiria wanaosafiri kutoka mataifa ya Misri , Morocco na nchi zingine sita zenye waislamu wengi.

Idara ya usalama wa nchi inasema kuwa watu wenye siasa kali wanatafuta mbinu za kuangusha ndege.

Mabomu yanaweza kufichwa ndani ya laptopu, tabiti, kamera, vifaa vya kucheza DVD na vya michezo ya eletroniki.

Marekani yapiga marufuku laptopu na tabiti kutoka mataifa 8

Sudan yapinga amri ya Trump

Jaji apiga marufuku amri ya Trump kurudisha wahamiaji makwao

Iraq kuondolewa kwenye Orodha ya Trump

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa mashirika tisa yakiwemo ya Egypt Air na Royal Air Maroc, yamepewa muda wa saa 96 kuanzia leo Jumanne kupiga marufuku vifaa vikubwa kushindasimu kutoka kwa ndege.

Haijatangazwa ni lini marufuku hiyo itafika mwisho.