Mtalii aliyepigwa picha akiwa na bunduki ya polisi azua ghadhabu Mexico

Mtalii aliyepiwa picha akiwa na bunduki ya polisi azua ghadhabu Mexico Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mtalii aliyepiwa picha akiwa na bunduki ya polisi azua ghadhabu Mexico

Watu nchini Mexico wameelezea ghadhabu zao baada ya picha ya mtaalii mmoja kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika bunduki ya afisa wa polisi.

Mtalii huyo anayetabasamu na ambaye hana shati anaonekana akiwa na polisi wawili waliosimama kando katika eneo la starere la Playa del Carmen.

Vyombo vya habari vilisema kuwa bunduki hiyo haikuwa na risasi.

Hata hivyo ni kinyume na sheria afisa wa polisi kusalimisha bunduki yake.

Jumla ya polisi 80 walitumwa eneo hilo hivi majuzi kukabiliana na visa vya uhalifu.

Mwezi Januari watu watano waliuawa eneo la Playa del Carmen, wakati mwanamume mmoja alifyatua risasi kwa klabu moja ya usiku wakati wa tamasha moja maarufu ya muziki,

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mtalii aliyepiwa picha akiwa na bunduki ya polisi azua ghadhabu Mexico