Uingereza yapiga marufuku laptopu ndani ya ndege kutoka nchi 6

Uingereza yapiga marufuku laptopu kwenye ndege
Image caption Uingereza yapiga marufuku laptopu kwenye ndege

Serikai ya Uingereza imatangaza marufuku ya laptopu kwa abiria wanaosafiri moja kwa moja kutoka Utuki, Lebanon, Jordan, Misri, Tunisia na Saudia Arabia, wakielekea nchini Uingereza

Marufuku hiyo pia inazuia vifaa kama tabiti na vifaa vya kucheza muziki vya kutumia DVD sawa na marufuku iliyotangazwa na Marekani.

Serikali ya Uingereza ilisema kuwa hii inafuatia mazungumzo yanayohusu usalama wa safari za ndege, ikisema kuwa marufuku hiyo inahitajika.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa mabomu yanaweza kufichwa ndani vifaa kadha.

Mashirika ya ndege ya Uingeeza yanayoathirika

Mashirika ya ndege ya kigeni yanayoathirika

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Uingereza yapiga marufuku laptopu kwenye ndege