Kocha aikacha Tp Mazembe

Tp Mazembe kocha Haki miliki ya picha Google
Image caption Thierry Froger kocha aliyebwaga manyaga

Klabu ya soka ya Tp Mazembe ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo inatafuta Kocha mpya wa kukinoa kikosi hicho baada ya kocha wao Mfaransa Thierry Froger, kuamua kuondoka klabuni hapo kwa hiari.

Kwa mujibu wa klabu ya Mazembe kocha huyu ameamua kuondoka baada ya kushindwa kufikia malengo ya kufika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa ambapo waliondolewa na timu ya Caps United ya Zimbabwe.

Mazembe ambao ni mabingwa wa klabu bingwa Afrika kwa mara tana wanatarajiwa kumtangaza kocha mpya kabla ya michezo ya mwezi April, ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Timu hiyo ya Congo inashiriki michuano ya kombe la shirikisho baada ya kungolewa kwenye michuano ya klabu bingwa na watacheza na timu ya JS Kabylie ya nchini Algeria.