Phil Jones kufanyiwa vipimo zaidi

PHIL JONES Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki Phil Jones wa pili kutoka kulia akiwa mazoezi jana kabla ya kuumia

Mchezaji wa timu ya taifa ya England Phil Jones, atasubiri kufanyiwa vipimo vya upigani picha ya x-rays.ili kuweza kujua ukubwa wa tatizo la kidole gumba alichoumia akiwa mazoezini.

Beki huyu ameshindwa kusafiri na kikosi cha timu ya taifa kinachokwenda Dortmund kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani .

Kocha wa kikosi cha England Gareth Southgate

" tumemrudisha Jones kataika klabu yake, tutajua zaidi baada ya vipimo katika saa 24 au 48 zijazo ."

Southgate hana mpango wa kumuita mchezaji mwingine kama mbadala ya beki huyo kwanza wataangalia hali yake baada ya mchezo wa kirafiki,katika kikosi chake ananjia mbadala ya mabeki wa kati ambao ni John Stones ,Michael Keane na Chris Smalling,