Tusk adaiwa kusaliti maslahi ya Poland

Donald Tusk amekuwa akipigwa vita na Poland ndani ya Umoja wa Ulaya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Tusk amekuwa akipigwa vita na Poland ndani ya Umoja wa Ulaya

Waziri wa ulinzi wa Poland, Antoni Macierewicz amemshutumu Donald Tusk kwa kusaliti maslahi ya nchi, kuhusu ajali ya ndege ya Smolensk iliyotokea mwaka 2010 na kugharimu maisha ya aliyekuwa Rais wa Poland Lench Kaczynski na watu wengine 95.

Bwana Tusk, ambaye sasa ni rais wa Umoja wa Ulaya, alikuwa waziri mkuu wakati huo.Macierewicz amekosoa uamuzi wa Tusk kuchagua Urusi kuongoza uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Adhabu inayotokana na uhaini wa kidiplomasia ni kifungo cha miaka 10 gerezani.

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Poland ana siku thelathini kuamua kama ufanyike uchunguzi kuhusu shutuma hizo.

Hizi ni jitihada mpya za chama cha Law and Justice katika kuharibu sura ya Tusk.Mapema mwezi huu Chama hicho kilipinga vikali kitendo cha Tusk kuchaguliwa tena kuongoza umoja wa ulaya kwa awamu ya pili.