Tsivangirai aonya wafuasi wake wataandamana kudai uchaguzi huru

Morgan Tsivangirai Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchaguzi wa awali ulitawaliwa na ghasia, vitisho na shutuma nyingi za wizi wa kura.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ameonya kuwa wafuasi wake wataingia mitaani kuandamana ikiwa madai yao ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki hayatatekelezwa.

Mujuru kuungana na MDC ili kumuondoa Mugabe

Sanamu mpya za Mugabe zazua ubishi Zimbabwe

Wapinzani waandamana leo Zimbabwe

Akihutubia wafuasi wake viungani viungani mwa eneo la biashara mjini Harari , Bwana Tsvangirai alilishutumu taifa kwa kupuuza haki ya waZimbabwe ya kupiga kura katika uchaguzi ujao wa urais na wabunge, wakati yeye na chama chake cha Movement for Democratic Change watakapojaribu tena kuumaliza utawala wa muda mrefu wa rais Robert Mugabe.

Uchaguzi wa awali ulitawaliwa na ghasia, vitisho na shutuma nyingi za wizi wa kura.

Mchungaji wa Zimbabwe aliyetambuliwa kwa kampeni yake ya #ThisFlag Movement - mchungaji Evan Mawarire pia aliuhutubia umati wa wafuasi wa Tsvangirai, akisema waZimbabwe hawana hofu tena.

Image caption Morgan Tsivangirai akihutubia mkutano wa wafuasi wake mjini Harare

Mahakama ilipuuzilia mbali mashtaka ya kutokuwa na utiifu dhidi ya mchungaji Mawarire mwezi Julai.

Bwana Mawarire amekuwa akijihusisha na kampeni ya mitandao ya habari ya kijamii ya kupinga namna serikali inavyoshughulikia uchumi wa nchi.

Wakati huo huo mshirika wa karibu wa zamani wa rais Robert Mugabe ametangaza kumuunga mkono hasimu wake Morgan Tsvangirai katika uchaguzi mkuu ujao.

Didymus Mutasa, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha Zanu-PF mnamo mwaka 2015, amesema anataka Bwana Tsvangirai kuongoza muungano wa upinzani dhidi ya Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 93, ambaye anawania kurefusha zaidi muda wake wa miaka 37 mamlakani katika uchaguzi huo