England yachapwa na Ujerumani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lukas Podolski akishangilia goli alilofunga

Timu ya taifa ya England imekubali kichapo cha bao 1-0 ugenini dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki.

Bao pekee la ushindi katika mchezo huo liliwekwa kambani na mshambuliaji Lukas Podolski katika dakika ya 69 ya mchezo kwa shuti kali la umbali wa mita 25 lilomshinda kipa wa England Joe Hart.

Mchezo huu wa kirafiki ulikua ni mchezo wa mwisho kwa mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ujerumani Lukas Podolski anayestaafu soka la kimataifa akiwa na umri wamiaka 31.

Lukas Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Podolski akirushwa juu na wenzake baada ya mchezo kumalizika ikiwa ni sehemu ya kuuga nyota huyo mwenye miaka 31

Mshambulia huyu alianza kuichezea timu ya taifa ya wakubwa mwaka 2004 na kufunga jumla ya magoli 49 katika michezo 130.