Matokeo ya michezo ya kimataifa

Steven Naismith Haki miliki ya picha PA
Image caption Mfungaji wa bao la kusawazisha la timu ya Scotland Steven Naismith

Baadhi ya timu za taifa za mchezo wa soka zimecheza michezo ya kirafiki ya kimataifa usiku wa kuamkia leo.

Scotland wakiwa nyumbani kwao wameambulia sare ya 1-1 na Canada ,Jamuhuri ya Czech imewatambia nyumbani Lithuania kwa kuwachapa mabao 3-0.

Cyprus wao wakautumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 - dhidi ya Kazakhstan, Cambodia wao wakalala nyumbani kwa kichapo cha mabao 3-2 toka kwa timu ya taifa ya India.

Djbouti wao wakawalaza Sudani ya kusini kwa maba 2-0, Yemeni wakafungwa katika uwanja wao wa nyumbani na Palestina kwa bao 1-0.