Marekani:kupambana na IS ni lengo letu la kwanza

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema wataangusha kundi la IS Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema wataangusha kundi la IS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson, ameuambia mkutano wa nchi 68 unaojumuisha muungano dhidi ya wanamgambo wa Islamic State kuwa kupambana na IS ni lengo lao la kwanza Mashariki ya kati.

Bwana Tillerson ameuambiamkutano jijini Washington kuwa Serikali ya Trump imedhamiria kuharibu ushirika wa magaidi:kiongozi wake Abu Bakr al- Baghdadi bila shaka atauawa.

Waziri huyo ameahidi kuwa Marekani itasaidia kuyaweka maeneo katika hali ya usalama kwa ajili ya kuwawezesha wale waliokimbia kurejea