Polisi:shambulio la London ni la kigaidi

Polisi wakiwa wamemzingira mtu anayeshukiwa kutekeleza shambulizi Haki miliki ya picha PA
Image caption Polisi wakiwa wamemzingira mtu anayeshukiwa kutekeleza shambulizi

Polisi jijini London wamesema shambulio la siku ya Jumatano katika daraja la Westminster na nje ya bunge la nchi hiyo yanaweza kuhusishwa na itikadi kali ya kiislamu.

Polisi mwandamizi kuhusu masuala ya ugaidi, Mark Rowley, pia amesema wanaamini wanaweza kumtambulia mshambuliaji wa tukio hilo, lakini hakutoa taarifa zaidi.

Raia watano wameuawa na wengine zaidi ya arobaini kujeruhiwa na mtu aliyevurumiza gari sehemu ya kupitia watu katika daraja la Westminister. Baadae kuingia katika viwanja vya bunge ambapo alimchoka kisu polisi kabla ya kupigwa risasi.

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May, amesema tukio hilo ni la kusikitisha na kutuma salamu zake za rambirambi ndugu wa wafiwa na kuwaombea waliojeruhiwa.