Watson,Bedene waanza vibaya Miami open

Dan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dan Evans akiwa uwanjani

Wachezaji watatu wa mchezo wa tenesi wa Uingereza Dan Evans, Heather Watson na Aljaz Bedene wamepoteza michezo ya raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Miami.

Mchezaji namba 43 Evans alipoteza kwa Mmarekani Ernesto Escobedo. Kwa seti mbili 7-5 0-6 6-3

Watson, ambae alifika raundi ya nne mwaka jana alipoteza kwa Mromania Patricia Maria, kwa seti tatu 7-6 (7-4) 6-1 kupoteza huko kwa Watson kutamshusha katika viwango vya ubora .

Nae Aljaz Bedene amekua mwingereza wa tatu kuchapwa katika katika michuano hiyo baada ya kupoteza kwa Ujerumani Jan-Lennard Struff kwa 7-5 4-0