Kenya yaanza kuuza dhamana zake kupitia simu

Bunge la Kenya
Image caption Bunge la Kenya

Idara ya fedha nchini Kenya imezindua hati ya dhamana kwa jina Akiba, inayowalenga wawekezaji wadogo ambao wataweza kuzinunua kupitia simu zao kwa bei ya chini.

Je dhamana hizo hufanya kazi vipi?

Aly Khan Satchu, mchanganuzi wa maswala ya fedha na mkurugenzi wa kampuni ya Rich Management mjini Nairobi aliambia BBC ni kwa nini anaona hatua hiyo ni hatua kubwa ya kimaendeleo.

Maxence Melo apewa dhamana Dar es Salaam

-Inamruhusu mtu yeyote aliye na simu nchini Kenya kununua na kuuza dhamana hiyo kupitia simu hizo.

-Inaleta demokrasia katika soko la fedha. Inawapatia Wakenya uwezo wa kumiliki dhamana za serikali

-Watu walio na hadi dola 30 wana uwezo wa kuwekeza katika soko la hisa

Mfumo wa benki wa Kenya umetawaliwa na ulipaji wa fedha kupitia simu.

Kampuni ya Safaricom inatoa hudumu ya malipo M-Pesa ambayo ina wateja wapatao milioni 20 pamoja na vibanda mara 100 vya M-Pesa kwa kuwa ndivyo vinavyotumiwa sana kutoa fedha nchini humo.

Waziri wa fedha Henry Rotich amesema kuwa serikali ilikuwa imewasilisha ombi la shilingi milioni 150 ili kujaribu dhamana mpya ifikiapo mwezi Juni.