Mtu aliyetekeleza shambulio Uingereza ni Khalid Masood

Mshukiwa wa shambulio hilo ametambulika kuwa Khalid Masood
Image caption Mshukiwa wa shambulio hilo ametambulika kuwa Khalid Masood

Mtu ambaye polisi wanaamini alihusika na shambulio la kigaidi katika eneo la Westminister ametambuliwa rasmi kuwa Khalid Masood, kulingana na wapelelezi wa Scotland Yard.

Masood mwenye umri wa miaka 52 alizaliwa katika eneo la Kent na wapelelezi wanaamini kwamba alikuwa akiishi Midlands magharibi.

Masood hakuhusishwa katika uchunguzi wowote na hakuna ripoti yoyote ya upelelezi kuhusu mipango yake ya kutaka kutekeleza shambulio, kulingana na polisi.

Hatahivyo, alitambuliwa na polisi na kwamba alikuwa ameshtakiwa kwa kushambulia watu ikiwemo umiliki wa silaha na kusababisha taharuki mbele ya uma.

Hajashtakiwa na makosa yoyote ya ugaidi

Mtu yeyote mwenye habari kuhusu Masood anawezakuziwasilisha katika nambari ya simu ya kikosi cha kukabiliana na ugaidi- 0800 789 321