Wyclef Jean ashukiwa kimakosa kuwa mwizi Los Angeles

Wyclef Jean ashukiwa kimakosa kuwa mwizi Los Angeles Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wyclef Jean ashukiwa kimakosa kuwa mwizi Los Angeles

Mwanamuziki Wyclef Jean amewalaumu polisi huko Los Angeles, Marekani, kwa kumshuku kuwa mwanamume ambaye aliiba kutoka kituoa cha mafuta kilichokuwa karibu.

Mwanamuziki huyo raia wa Haiti, alichapisha video yake kwenye mtandao wa twitter akisimama karibu la gari la polisi baada ya kufungwa pingu.

Alidai kuwa polisi wa Los Angeles walimfunga pingu bila ya sababu yoyote lakini idara hiyo ya polisi ilikana kufanya hivyo.

Wyclef Jean anafahamika vyema kuwa moja wa waanzilishi wa kundi la rap la Fugees na ameshirikiana na wanamuzi kama Shakira, Timbaland na Lil' Kim.

Anasema alikuwa kwenye sudio na mwanamuziki T-Baby wakati kituo cha mafuta kilipopowa, na kudai kuwa alisimamishwa na polisi baadaye kwa sababu alikuwa mtu mweusi ambaye alikuwa amefunga bandana iliyokuwa ikifanana na mtu aliyepora kituoa cha mafuta.

Akiongea na BBC msemaji wa idara ya polisi wa Los Angeles alisema kuwa Wyclef Jean, alikuwa kwenye kiti cha abiria kwenye gari lililokuwa likifanana na lile lilotumika kwenye wizi.

Polisi walisema kuwa walimwachilia bila ya kumfungulia mashtaka.