Maelfu ya watu wahamishwa kufuatia mlipuko kwenye ghala la silaha Ukraine

Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha Ukraine Haki miliki ya picha Ukraine government
Image caption Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha Ukraine

Karibu watu 20,000 wanahamishwa kufuatia kutokea kwa misururu ya milipuko kwenye ghala kubwa la kuhifadhia silaha mashariki mwa Ukraine, kisa ambacho kimetajwa na maafisa kuwa cha kuhujumu.

Ghala hilo lililo eneo la Balakliya liko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka eneo la mapigano na waasi wanounga mkono Urusi.

Hutumika kuhifadhi maelfu ya tani za risasi na makombora.

Makundi ya uokoaji yanaongoza shughuli kubwa ya kuwahamisha watu wanaoishi katika mji huo na vijiji vilivyo karibu.

Eneo lote la ghala hilo lina ukubwa wa karibu hekari 350.

Haki miliki ya picha DSNS
Image caption Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha Ukraine

Silaha kutoka ghala hilo hutumiwa na vikosi vilivyo eneo la mzozo katika maeno yaliyo karibu ya Luhanks na Donetsk.

Mamlaka inachunguza sababu tofauti zilizosababisha milipuko hiyo. Waziri wa ulinzi Stepan Poltorak alisema kuwa kuna uwezekano wa kifaa kinacholipuka kuangushwa na ndege isiyokuwa na rubani.

Ndege isiyokuwa na rubani inaripotiwa kutumika kujaribu kuwasha moto kwenye ghala hilo mwezi Disemba mwana 2015.

Zaidi ya watu 9,700 wameuawa kwenye mzozo ambao ulilipuka mwaka 2014 wakati Urusi ilimega rasi ya Crimea.

Image caption Maelfu wahamishwa baada ya mlipuko kwenye ghala la silaha Ukraine