Shambulio la London: Saba wakamatwa baada ya uvamizi wa polisi

Maafisa wa polisi wa uchunguzi wa mwili katika daraja la Westminster Bridge Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maafisa wa polisi wa uchunguzi wa mwili katika Westminster Bridge

Watu saba wamekamatwa katika uvamizi mjini London na Birminghamkufuatia shambulio la Westminster lililowauwa watu wanne, kwa mujibu wa polisi.

Mamia ya polisi wa upelelelezi wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha wakifanya uchunguzi dhidi ya makazi sita, amesema kaimu naibu wa kamishna wa polisi Mark Rowley.

Wale waliokufa walikuwa ni mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 40, mwanamume mwenye miaka 50 Polisi Keith Palmer pamoja na mshambuliaji, aliongeza.

Saba miongoni mwa majeruhi bado wako hospitalini katika hali mahututi.

Wengine 29 zaidi wamekuwa wakipata matibabu hospitalini, ameongeza Rowley.

Katika shambulio la Jumatano, mwanamume mmoja aliendesha gari kwenye njia ndogo karibu na Westminster na kuwagonga wapitanjia, huku akiwaacha kadhaa na majeruhi.

Kisha alimdunga kisu polisi na akapigwa risasi na polisi kwenye eneo la bunge.

katika kauli iliyotolewa nje ya Scotland Yard, Bwana Rowley alisema : "Uchunguzi uliofanyika mjini Birmingham, London na maeneo mengine ya nchi unaendelea .

"Bado ni imani yetu inayoendelea kutokana na uchunguzi -kwamba mshambuliaji huyu alifanya shambulio hilo peke yake na alijifunza kutokana na ugaidi wa kimataifa

"kwa sasa hatuna taarifa za kipekee juu ya vitisho zaidi vya mashambulio kwa umma ."

Amesema bado hatayataja majina yawaathiriwa waliokuwa kwenye daraja , ambao walikuwa "raia wa mataifa mabli mbali", na amewataka wandishi wa habari kutotangaza jina la mshambuliaji wakati misako ikiendelea.

Amesema wakazi wa London watarajie kuwaona maafisa zaidi wa polisi mitaani, baada ya likizo za polisi kuahirishwa na kuongezwa kwa muda wa saa zao za kazi.

Awali ilidhaniwa kuwa watu watatu waliuawa katika daraja Westminster Bridge, lakini bwana Rowley ameelezea kuwa walikuwa ni wawili tu katika kauli yake.

Haki miliki ya picha HoC
Image caption Wabunge walisimama kwa muda wa dakika moja kimya bungeni kabla ya kuanza shughuli zao za kawaida za siku

Waziri wa Ulinzi Sir Michael Fallon amekiambia kipindi cha BBC Radio 4 'cha leo kwamba "dhana ya kikazi" ni kwamba mshambuliaji alikuwa na uhusiano na '' magaidi wa kiislam kwa kiasi fulani". Alitoa rambi rambi zake kwa bolisi Pc Palmer, aliyekuwa na umri wa miaka 48 baba na mume ambaye alikuwa katika kikosi kisichukuwa na silaha cha ulinzi wa Bunge na mabalozi aliyehudumu kwa miaka 15 katika kikosi hicho.

Pc Palmer alimzuwia mshambuliaji kuingia ndani ya Bunge na "kutoa maisha yake kwa ajili ya demokrasia tunayoithamini", alikiambia kipindi cha asubuhi cha BBC.

Alipoulizwa kuhusu hali katika mji wa London, Sir Michael alisema: "London inarejea katika hali yake ya kawaida. Waliwahi kuuona ugaidi kama huu kabla na hawawezi kuuruhusu uwateteleshe.

Haki miliki ya picha AFP

Brendan Cox, mumewe mbunge aliyeuawa - Jo Cox, amesema kuwa ni muhimu kukumbuka kuwa "hii ni hadithi juu ya watu ambao hawakuja nyumbani jana".

Waziri Mkuu Theresa May, ambaye atatoa taarifa muda mfupi ujao , amesema kuwa shambulio " halikuwa na sababu wala maana '' katika mji mkuu , na jaribio kama hilo la kuharibu maadili ya Uingereza "litashindwa daima".

Rais wa Marekani Donald Trumpalikuwa mmojawapo wa viongozi wa dunia kutangaza uungaji mkono wao, akituma ujume wa Tweeter "Nimeongea na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May leo kumpa rambirambi kufuatia shambulio la ugaidi mjini London . Yuko imara na salama kabisa ."

Shambulio la mauaji ya watu wengi katika eneo la Westminster Bridge na ndani ya eneo la Bunge ni jambo ambalo awakuu wa usalama nchini Uingereza wamekuwa wakijiandaa kukabiliana nalo kwa muda.

lengo la magaidi si kuuwa tu na kukata viungo-bali pia kusababisha mkanganyiko na hali ya kuchanganyikiwa ambayo itaathiri imani na misingi ya taifa.

Na mshambuliaji huyu alitaka kufanya hivyo kwa kutumia teknolojia ya chini iwezekanayo.

Nyakati ambazo magaidi walitumia mbinu kubwa, mabomu makubwa na kufanya mipango ya mashambulio zimekwisha: Mashirika ya usalama ya kimagharibi - hususan lile la MI5 na washirika wake - ni wazuri sana katika kubaini njama hizo na kuzivuruga.

kadri inavyochukua muda kupanga shambulio la aina hiyo, ndivyo watu zaidi wanavyohusika, na ndivyo fursa ya huduma za usalama kutambua ni nini kinachoendelea zinavyoongezeka.