Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa Haki miliki ya picha Hankook Daily via Getty Images
Image caption Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Feri imeinuliwa kutoka baharini, miaka mitatu tangu izame katika moja ya janga baya zaidi nchini Korea Kusini.

Feri hiyo ya Sewol ilizama nje ya kisiwa kilicho kusini magharibi cha Jindo, tarehe 16 mwezi Aprili mwaka 2014 na kuwua watu 304 wengi wao wakiwa ni watoto wa shule.

Feri hiyo inatarajiwa kufikishwa bandari chini ya wiki mbili ambapo familia za waathiriwea zitaisubiri.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Miili ya waathiriwa 9 inaaniwa kukwama ndani ya feri iyo na kuiinua kutoka bahari ilikuwa moja ya matakwa ya familia zao.

Serikali iliitikia shinikizo za kukiiinua chombo hicho chenye uzito wa tani 6,825 katika moja ya oparesheni ngumu zaidi kuwai kufanywa,

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Binti wa umri wa miaka 16 wa Huh Hong Hwan alikuwa mmoja wa waathiriwa ambaye mwili wake haukupatikana

"Kwa kuiona Sewol, siwezi kueleza vile ninavyohisi sasa," bwana Hu aliliambia shirika la AFP alipoitazama feri hiyo ikiinuliwa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Ajali hiyo ilisemekana kusababishwa na sababu tofauti ikiwemo feri kuundwa kwa njia mbaya na wahudumu kutokuwa na ujuzi wa kutosha.

Nahodha wake alihukumiwa kifungo jela kwa mashtaka ya kuua.

Haki miliki ya picha Reuters/Korea Coast Guard
Image caption Feri iliyozama nchini Korea Kusini miaka 3 iliyopita na kuwaua watu 304 yainuliwa

Ghadhabu kutokana na jinsi serikali ilishughulikia janga hilo zilichangia kushuka kwa umaarufu wa rais wa zamani Park Geun-hye ambaye alitimuliwa madarakani juzi.